Social Icons

Monday 10 February 2014

Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar chafanya sherehe za mahafali ya tano


01
Mkurugenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Bi. Zulekha Khamis Omar akitoa maelezo juu maendeleo ya Chuo katika Mahafali ya tano Chuoni hapo.
02
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Khamis Mussa Omar akieleza machache kuhusu muelekeo wa Chuo hicho na kumkaribisha Mgeni rasmin kutunuku vyeti kwa wahitimu.
03
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizunguza na wahitimu mbalimbali (hawapo pichani) mara baada ya kuwatunuku vyeti na stashahada katika Mahafali ya tano Chuoni hapo, (kulia yake) Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Khamis Mussa Omar na (kushoto) Kaimu Mwenyekiti Bi. Naila Jidawi.
04
Baadhi ya wahitimu wa Mapishi ya vyakula na Uokaji wakiwa wamesimama mara baada ya kutunukiwa vyeti na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk katika sherehe zilizofanyika Chuoni hapo. 
 05
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika sherehe ya Mahafali ya tano ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii  Maruhubi Zanzibar. 

No comments: