AMA KWELI
MGANGA HAJIGANGI
WANAFUNZI
wanaosomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(Muhas) wanaishi katika mazingira hatarishi kwani wanaweza kupata magonjwa ya
mlipuko na yale ya kuambukizwa wakati wowote.
Uchunguzi
uliofanywa na Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ndani ya
majengo ya chuo hicho yaliyo karibu na taasisi ya mifupa (MOI), umegundua
kwamba kwa miezi mingi, vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi hao vimejaa na kuziba
kabisa, hali inayowafanya vijana hao, licha ya kushindwa kupata huduma hiyo
muhimu ya kibinadamu, pia kuwa katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya mlipuko.
“Hali ni
mbaya sana hapa kwa kweli. Hatuna huduma ya choo kwa miezi miwili hadi mitatu
sasa, tunapobanwa na haja, hasa kubwa, hulazimika kukimbilia Kariakoo kwenye
vyoo vya kulipia, hapa hapafai,” mmoja wa wanachuo hao aliiambia OFM na kuomba
hifadhi ya jina lake.
Wanafunzi
hao ambao walitoa ushirikiano wa kutosha kwa makachero wetu, pia walisema
majengo mengi yanayotumiwa kama mabweni yao ya kulala, yamechakaa na hivyo
kuwafanya wawe na hofu kubwa, kwani yanaweza kuanguka wakati wowote.
OFM
ilishuhudia ngazi za kushuka na kupanda, zinazozunguka nje ya majengo hayo
zikiwa zimechakaa vibaya huku vyuma vilivyowekwa pembeni kwa ajili ya
kujishikilia vikiwa vimemongonyoka. Ni hatari kama likitokea tukio la ghafla,
mfano wa moto, litakuwa ni jambo gumu kwao kuweza kujiokoa kupitia ngazi za
nje. Hata baadhi ya milango inayotokeza nje ya ngazi hizo katika maghorofa
hayo, imefungwa kutokana na ubovu.
Licha ya
kero hizo, pia wanafunzi hao walilalamikia kitendo cha kujazana kupita kiasi
katika vyumba vyao vya kulala, kwani wamepangwa hadi wanane katika chumba
kimoja.
Baada ya
kutoka kwenye chumba cha madenti hao (majina tunayo) OFM ilitua kwenye jengo
moja ambalo liliwahi kulipuka kwa moto lakini bado limechakaa kutokana na
kutofanyiwa ukarabati.
MSEMAJI WA
MUHIMBILI ABANWA, AKISALITI CHUO
Baada ya
OFM kunasa uozo huo ndipo ilipoamua kuwasiliana na msemaji wa Muhimbili, Amiela
Angelekera.
OFM:
Habari za leo kiongozi?
AMINIELA:
Salama tuu, za kwako? Samahani naongea na nani?
OFM:
Unaongea na Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers.
AMINIELA:
Ok, nikusaidie nini?
OFM:
Unafahamu kama vyoo vya hosteli ya wanafunzi vyote vimejaa? Je, kuna mkakati
wowote wa kurekebisha maana ni miezi mingi imepita.
AMINIELA: Mmmh..(anaguna
kidogo) sijajua ni vyoo vipi, unatakiwa uwe mwandishi mzuri wa taaluma yako
unapozungumzia chuo, njoo twende wote tukaone hivyo vyoo.
OFM:
Taaluma ipi ambayo unadhani hawana OFM? Tayari tumefika hapo na kujionea ubovu
wa miundombinu ambayo inahatarisha maisha ya wanafunzi na chuo kwa ujumla.
AMINIELA:
Nimesema njoo ofisini kwangu, maana sipendi kuzungumza kwenye simu ishu kama
hizi, kwanza mimi sihusiki na chuo maana ni taasisi nyingine.
OFM: Ok,
kwa nini umelizungumzia suala hilo.
AMINIELA: Sihusiki
na chuo, hiyo ni taasisi nyingine.
OFM: Ok,
sawa kazi njema.
source: GPL
No comments:
Post a Comment