Social Icons

Friday 1 November 2013

SHEREHE ZA MAHAFALI YA 11 CHUO KIKUU KAIRUKI



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof. Keto Mshigeni, anapenda kuwaalika wahitimu wote wa mwaka wa masomo wa 2012/2013, wazazi, walezi wadau mbalimbali, wananchi na waandishi wa habari,  kwenye sherehe za Mahafali ya Kumi  na Moja, zitakazofanyika Jumamosi, tarehe 2 Novemba 2013, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, kuanzia Saa 3:30 Asubuhi.

Mgeni rasmi atakuwa ni Mkuu wa Chuo, Mheshimiwa Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye pia atatunuku vyeti, shahada, na stashahada kwa wahitimu.

Wananchi wote mnakaribishwa kwenye mahafali hayo.
Tangazo hili limetolewa na:
                  Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo,
      Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki,
S.L.P.  65300, Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2700021/4, Mob:0764378755

        Faksi: +255 22 2775591,  Barua pepe: secvc@hkmu.ac.tz   


No comments: