Social Icons

Wednesday 22 May 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA NANE YA KAMISHENI YA VYUO VIKUU MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM




  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali, yatakayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yamefunguliwa leo. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR
Baadhi ya washiriki  wa maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufungua rasmi maonyesho hayo ya siku tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Maofisa wa mfuko wa PPF, kutoka (kushoto) ni Meneja wa Kanda ya Ilala, Evans Musiba, Meneja Uhusiano, Lulu Mengele na Ofisa Masoko, Sereki Michael, wakati alipotembelea katika banda la maonyesho la PPF, leo kwenye maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

PICHA NA OFISI YA MAKAM WA RAIS

No comments: