Mgeni Rasmi wa hafla ya mahafali ya pili ya Chuo cha Ualimu Moravian kilichopo Mtaa wa Forest ya Zamani jijini Mbeya Dr Victoria Kanama, ambaye ni Mkurugenzi wa Hospitali ya K'S iliyopo jijini hapa na pia ni Mkuu wa Bodi ya Chuo Kikuu cha TEKU, akimkabidhi mmoja wa wahitimu cheti chake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Bwana David Mwankina (kushoto), akifuatiwa na Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Alinikisa Cheyo, Mgeni rasmi Dr Victoria Kanama na Mkuu wa Chuo hicho cha Ualimu Eliackim Mtawa.
Wahitimu wakiingia kwa maadamano katika Sherehe za mahafali ya pili ya Chuo chao yaliyofanyika katika Chuo cha Ualimu Kilichopo Mtaa wa Forest ya Zamani Jijini Mbeya.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapinduzi wakiimba katiak sherehe hizo, ambayo ni shule inayotumiwa na Wanachuo wa chuo hicho kwa mazoezi ya kufundisha.
Wanachuo wa Mwaka wa pili wa chuo hicho wakionesha umahiri wa kucheza miondoko ya Kwaito
Mkuu wa Chuo hicho Eriackim Mtawa akitoa taarifa ya chuo hicho katika mahafali ya pili yaliyofanyika Mei 2 mwaka huu chuoni hapo ambapo kati ya wanafunzi 103 kati ya 104 kwa mwaka uliopiata walifaulu.
Wanafunzi wa Shule ya Mapinduzi wakionesha ingizo la ufundishaji bora, wakiwataka walimu kufuata maadili ya kazi yao.
Wahitimu wakiimba wimbo wa kuaga katika Mahafali ya pili yaliyofanyika Mei 2 mwaka huu chuoni hapo.
Baadhi ya wazazi na walezi wa wahitimu waliohudhuria katika mahafali ya pili ya chuo hicho.
Waandishi wa habari waliohudhuria katika mahafali hayo Bwana Richard Mwafulirwa (kushoto).
Mwalimu Timoth Mwanjwango wa Chuo cha Ualimu cha Moravian, aliyepata tunzo baada ya wanafunzi wake kufanya vizuri kwa kufaulu alama "A" katika mtihani wa Taifa kupitia somo la Sayansi Jamii.
(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya).
No comments:
Post a Comment