Social Icons

Sunday, 15 January 2012

IBADA MAALUMU YA KUOMBEA MITIHANI KESHO YAFANA KATIKA CHUO CHA MIPANGO DODOMA

Baadhi ya waumini wa Kanisa laKiinjili la Kilutheri Chuo cha Mipango Dodoma wakiwa kwenye ibada ya kuombea mitihani inayotarajiwa kuanza kesho kwaajili ya kumalizia mhula kwa kwanza.
Pia tulipokea ugeni kutoka Usharika mama wa Mnadani, ambapo watoto hawa waliamua kucheza kiduku cha k-church- church mambo ya kisasa nayo!!!
Mbele ya mtihani kila goti litapigwa mbele zake kuomba msaada na ulinzi wa kiroho!!1 hapa miongoni mwaotangu wajiunge na chuo hawajawahi kusali lakini ibada ya leo ilikuwa muhimu kwaokwaaajili ya kesho, mungu tambua mahitaji yao kwa kadiri waombavyo wasaidie wasirudi kwenye semina elekezi!!!(siku hizi hawaiti supplimentary)


Wakitakiana kilalakheri mara baada ya kutoka kwwenye ibada hiyo , huku pembeni kuna basi la chuo kikuu cha Dodoma UDOM ambalo limekuwa likipata hifadhi chuo cha mipango daily
Mchungaji wa Usharika wa Mnadani ambaye aliongoza ibada hiyo akiwa na mhubiri anayetoa huduma katika vyuo vya elimu ya juu Mkoani Dodoma Fanuel Kyombo ambaye alipigilia misumari ya kujenga confidence kwenye mitihani,akinadada waache kutumia miili yao vibaya kama njia ya kuongeza marks kwenye mitihani yao !! akina kaka mambo ya phantom noooooooo!!!
Darasa lilizidiwa ikabidi wengine wabaki nje baada ya theatres zote kufungwa kwa maandalizi ya kitu examinations kuanzia kesho hadi 26 Feb
Nami kibarua wenu wasomaji nitakuwa kwenye kimbembe hicho hicho kuanzia kesho kwenye ukumbi unaoonekana nyuma yangu hapa, naomba maombi yenu,nimejiandaa na nipo happy kukutana na rafiki yangu mitihani nitasema naye mpaka anielewe!!!!


Picha zote kwa Hisani ya Dany Tweve wa Indaba Africa Blog



No comments: