Social Icons

Saturday 15 October 2011

Waziri Wa Elimu Azindua Bodi Mpya

Dkt.Shukuru Kawambwa


Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini VETA, imepewa changamoto mpya za kuongeza idadi ya nafasi za mafunzo katika vyuo vyake, ili kutoa fursa kubwa zaidi kwa wanafunzi wengi zaidi, kufaidika na mafunzo yatolewayo na vyuo vya VETA, kote nchini.
Changamoto hizo, zimetolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini, Dr. Shukuru Kawambwa, alipokuwa anazindua bodi mpya ya VETA, katika hafla fupi, iliyofanyika VETA Makao Makuu, eneo la Changombe, hapa jijini Dar es Salaam.
Dr. Kawambwa ameitaka bodi hiyo ya VETA, kuweka mipango mkakati madhubiti inayopimika na unaotekelezeka ndani ya miaka mitatu ili kuelekeza rasilimali zake kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.
Pia Dr. Kawambwa ameitaka bodi hiyo, kupanua wigo wa mafunzo inayoyatoa,, kuyaimarisha kwa kuyaboresha kwa viwango vya kimataifa na kuzingatia uwiano wa kijinsia katika kutoa nafasi za mafunzo.
Awali, akimkaribisha Waziri kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Eng. Zebadiah Moshi, amemshukuru Rais Kikwete kwa uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi mzoefu, na kumshukuru Waziri kwa kumpatia wajumbe wa bodi makini na mahiri ambao wataiondoa VETA kutoka hapo ilipo na kuifikisha kule inakotarajiwa kufika.
Naye, Mwenyekiti wa bodi hiyo mpya ya VETA, Prof. Idrissa Mshoro, alimshukuru waziri, na kumuahidi kuwa bodi yake, itazitekeleza changamoto zote zilizotolewa na Waziri kwa ukamilifu kabisa.

Bodi hiyo mpya yenye wajumbe 12, ni bodi ya sita tangu kuundwa kwa VETA, na itakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu


No comments: