Social Icons

Monday 17 October 2011

WAREMBO WA CHUO KIKUU CHA KAMPALA KUTOANA JASHO JUMAMOSI HII

Shindano la kumsaka mrembo wa chuo kikuu cha Kampala International University 2011 linatarajiwa kufanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Savanna Lounge (quality center) uliopo barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam.
jumla ya warembo 12 watachuana vikali kuwania taji hilo siku ya tarehe 22 octoba.
Shindano litapambwa na wasanii wa kizazi kipya ambao ni Dully sykes,D-nob,Ngoma za asili na vijana wa kutikisika(shekrs),mbali ya burudani hizo kutakuwa na suprize ya majaji pamoja masupastaa wa movie.
Miss Kampala Internationa 2011 imeandaliwa na serikali ya wanafunzi wa chuo hicho ikishirikana na wadau maarufu wa mambo ya urembo na mitindo nchini Tanzania,tiketi za fainali hizi zinapatikana CLOUDS fM,CHUONI KWAO,JB BELMONT HOTEL,SAVANNA LOUNGE(quality center)kitchen hut (mlimani city) kwa iasi cha 10,000/= (regular) na V.I.P 30,000/=

No comments: