Social Icons

Tuesday 13 September 2011

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WALIOPATA AJALI YA MELI ZANZIBAR KUTOKA KWA WATANZANIA WANAOSOMA NANJING NORMAL UNIVERSITY NCHINI CHINA

.Sisi wanafunzi tunaosoma Nanjing Normal University nchini china tumepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za msiba mzito uliolikumba taifa letu la Tanzania,kutokana na kuzama kwa meli ya Mv spice Islander huko Nungwi zanzibar usiku wa tarehe 10 september 2011. Tunapenda  kutoa salamu zetu za rambirambi kwa kuungana na ndugu,jamaa ,marafiki wa Marehemu,na Watanzania wenzetu ,bara na visiwani  katika  kipindi hiki kigumu .
Ili kueleza majonzi na masikitiko yetu  makubwa katika msiba mkubwa uliolikumba taifa Rambirambi hizi ziwafikie Viongozi wote na Wananchi wote wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Tunatoa pole sana kwa majeruhi na walionusurika katika ajali hii.Zaidi ya yote tunaungana na Watanzania wenzetu katika maombolezo, huzuni na kuwatakia rehema.Tunawaombea Marehemu wote,familia za marehemu ,pia wale majeruhi  wawe na afya njema na  wapate kupona haraka.
Bwana ametoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe
                                                                      
Imetolewa na:
Moshi Goodluck
Ghatty Chacha
(postgradute students)
AMEN!!

Hizi ni salam Maalum kabisa kutoka China

No comments: