Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Na Mwandishi Wetu Dodoma.
Mapema
Septemba 2016 kwa mara ya kwanza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye aliwasilisha kwa mara ya kwanza Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari na kuanza kujadiliwa na kutolewa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa Habari nchini.
Kwa
sasa Muswada huu unaendelea kujadiliwa na kuchambuliwa na Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake
Mhe. Peter Serukamba na baada ya mchakato huo kukamilka utapelekwa kwa
ajili kuanza kujadiliwa na wabinge.
Sasa
hoja yangu naielekeza katika kuangalia Muswada huu hasa katika sehemu
ya Tatu (c) Uthibitishwaji wa wanahabari kifungu cha 18 (1) na (2)
vinaelezea kuwa Mtu hataruhusiwa kufanya kazi za uandishi wa habari
isipokuwa kama mtu amethibitishwa na Sheria hii na (2) inasema mtu
ambaye anakusudia kufanya kazi ya uandishi wa habari ataomba
kuthibitishwa na Bodi kwa utaratibu wa maombi utakaoainishwa katika
kanuni.
Ukisoma
kifungu hiki na sehemu zake zote utaona kuwa lazima kutakuwa na vigezo
ambavyo mwandishi wa habari atapaswa kuwa navyo ili Bodi iweze
kumthibitisha kuwa mwandishi wa habari kamili na baadae kumpatia Press
Card.
Tukiangali
kwa mifano tu ya taaluma ambazo watu wake wanapata udhititisho kutoka
kwa Bodi zao utaona kuwa hata vigezo vyenye ngazi fulani ya kitaaluma na
kwa mfano wanasheria ili kudhititishwa kuwa mwanasheria na kupata mhuri
wa kuwa Wakili unabidi uwe na Shahada ya Kwanza ya Sheria na kufanya
baadhi ya mitihani ya kufuzu ili kudhitishwa.
Kwa
waandishi wa Habari pia tutegemee kuwepo kwa vigezo na masharti ambayo
kwa vitahitaji kuongeza elimu tulizonazo katia fani yetu na pia hili
litasababisha sasa vyuo vya uandishi wa habari na mawasiliano kutoa
elimu iliyo bora zaidi ili kuendana na mabadiliko haya.
Tumeshudia
uwepo wa vyuo vya uandishi wa habari kila sehemu hata vingine
ukiangalia mazingira yake lazima utilie shaka kama vinatoa ile elimu
inayostahili na iliyodhibitishwa na mamlaka zilizopo za TCU na NACTE.
Niwaombe
tu wahusika katika vyuo vya uandishi wa habari kuzingatia vigezo na
masharti ya utoaji wa elimu ya Habari na Mawasiliano katika vyuo vyao
kwani kuja kwa Sheria ya Huduma za Habari ni mwanzo wa kuifanya taaluma
ya habari kuwa taalum inayoheshima na kuwa taaluma inayoheshimika sana
na sio rahisi kuipata kama sasa watu wanavofikiria tu ukitaka kuwa
mwandishi wa habari unaweza kusoma miezi mitatu hivi basi umekuwa
mwandishi wa habari.
Ingawa
kuna baadhi watu wanasema wanatumia vipaji vyao vya uandishi wa habari
na utangazaji lakini tujue kuwa kipaji bila ya kuendelezwa ni kazi bure
tunahitaji kuviendeleza vipaji hivyo kwa kupata elimu na ujuzi zaidi wa
fani ya habari ili kuendana na mabadiliko ya teknlolojia na Sheria za
nchini.
No comments:
Post a Comment