Katika
kuhakikisha kunakuwa na wasomi ambao wanakuwa na elimu kuhusu kodi,
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya uzinduzi wa Jumuiya ya Wanafunzi
wa Kodi (Student Tax Association) katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM) ambapo wanachama hao watatumika kutoka elimu kwa wananchi wengine
kuhusu kodi.
Akizungumza
katika uzinduzi wa jumuiya hiyo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema malengo ya kuwa na jumuiya za
kodi vyuoni ni kuwezesha jamii kupata elimu ya kutosha kuhusu kodi
kupitia wanachama wa jumuiya hizo ambao watakuwa wakipatiwa mafunzo
kuhusu umuhimu wa kulipa kodi lakini pia kuhudhulia midahalo mbalimbali
ambayo itakuwa inazungumzia kodi.
Alisema
hatua ya kuanzisha jumuiya hizo imekuja baada ya kuwa na vilabu katika
shule za msingi na sekondari nchini na sasa wakaona kuna umuhimu wa kuwa
na wanachama kutoka vyuo vya elimu ya juu ili wawe mabalozi wa TRA ili
kusaidia utoaji wa taarifa kuhusu kodi lakini pia na wao kutambua
umuhimu wa kodi ili hata baada ya masomo yao waweze kuwa walipa kodi
wazuri.
Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo akizungumza
na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa uzinduzi wa
Jumuiya ya Wanafunzi wa kodi chuoni hapo (Student Tax Association).
"Tulianzisha
mfumo wa vilabu mwaka 2008 ambapo tuna vilabu 195 kwa Tanzania Bara na
Zanzibar na katika vilabu hivyo tuna wanachama 15,520 hivyo tukaona sasa
ni muhimu kuwa na wanachama kutoka vyuoni ili nao waweze kupata elimu
kuhusu kodi,
"Wanachama
wa jumuiya hizi watakuwa na shughuli ya kutoa elimu kwa watu wengine
ambao hawana elimu ya kodi, kuandaa wataalum wa elimu ya kodi kwa miaka
ya baadae na hata walipa kodi wa baadae kwani tayari watakuwa wanafahamu
umuhimu wa kodi kwa maendeleo ya taifa," alisema Kayombo.
Makamu
wa Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM (ISTA), Amon Ojode
akielezea jinsi ambavyo wanafunzi wa IFM watanufaika na uwepo wa jumuiya
hiyo chuoni hapo.
Nae
Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM, Amon Ojode alisema
kuwa ni fursa ya kipekee kwa wanafunzi wa chuo hicho kupata nafasi ya
kuwa na jumuiya ya kodi na zaidi ni wanafunzi ambao wanajifunza masomo
yanayohusiana na kodi hivyo wanaamini watakuwa wawakilishi wazuri wa
TRA.
Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo akizungumza
na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa uzinduzi wa
Jumuiya ya Wanafunzi wa kodi chuoni hapo (Student Tax Association).
Waziri
wa Afya na Mambo Yote kwa Ujumla katika serikali ya wanafunzi wa IFM
(IFMSO), Suleiman Kahumbu akizungumza katika uzinduzi huo.
Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Diana Masalla akizungumzia kodi wakati wa uzinduzi wa jumuiya hiyo.
Baadhi
ya wanachama wa Jumuiya wa Wanafunzi wa Kodi IFM na wanafunzi wa chuo
hicho waliohudhuria uzinduzi wa jumuiya chuoni hapo.
No comments:
Post a Comment