Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akimsalimia mwanafunzi wa Udhamili katika Takwimu Rasmi Happiness Katuma wakati akikagua baadhi ya vitu mbalimbali kama maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akipitishwa katika maeneo mbalimbali ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kama maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa chuo hicho na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akiangalia vitabu mbalimbali vilivyopo katika maktaba ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda
akimwelezea Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal kuhusu chumba cha
kompyuta kilichopo chuoni hapo wakati wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini
ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu
Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe
28 Machi, 2015.
Na Veronica Kazimoto,
Dar es Salaam,
17 Machi, 2015.
Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimekamilisha
maadalizi ya kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam
wa Takwimu na Chuo cha Takwimu cha nchini India.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu
wa Chuo cha EASTC Prof. Innocent Ngalinda amesema mkataba huo utasainiwa tarehe
28 Machi, 2015.
“Maandalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya
Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo cha Takwimu cha nchini India
yamekamilika kwa kiasi kikubwa na ndio maana hapa mbele yenu mnamuona Naibu
Balozi wa Ubalozi wa India hapa nchini amefika kwa ajili ya kujirizisha”,
amesema Prof. Ngalinda.
Prof. Ngalinda amesema kuwa mkataba huo una manufaa makubwa kwa
kuwa utasaidia kuongezeka kwa wataalam wengi katika tasnia ya takwimu hapa
nchini.
Pamoja na ongezeko la watalaam wa takwimu hasa wakufunzi, kutakuwa
na ukarabati wa miundombinu katika chuo hicho ambapo mabweni ya wanafunzi
pamoja na ofisi za chuo hicho zitakarabatiwa.
Prof. Innocent Ngalinda amefafanua kuwa katika mkataba huo,
kutakuwa na mpango wa kubadilishana wanafunzi katika vyuo hivyo viwili ili
kupanua uelewa wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi zaidi katika
masuala ya kitakwimu.
Kwa upande wake Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal
amefurahishwa na maandalizi yaliyofanyika na kusema kuwa nchi yake iko tayari
kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa Takwimu
kutoka chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na chuo cha Takwimu cha nchini
India.
“Nimefurahishwa na maandalizi yaliyofanyika katika chuo hiki na
sasa tunamsubiri Waziri wa mambo ya Nje wa nchini India kwa ajili ya kutiliana
saini ya mkataba huu ifikapo tarehe 28 Machi, 2015,” amesema Naibu Balozi
Humpal.
Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni
jijini Dar es Salaam na chuo cha Takwimu cha India vimekuwa vikishirikiana
tangu mwaka 2012 lakini ushirikiano huo haukuwa rasmi hivyo vyuo hivyo vimeamua
kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili kufanya ushirikiano huo kuwa rasmi.
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
No comments:
Post a Comment