Social Icons

Monday, 3 February 2014

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NA CHUO KIKUU CHA TUMAINI WASHIRIKI KATIKA KUPITIA FOMU ZA KUCHUJA WATAKAOINGIA KATIKA KATIKA USAHILI WA SHINDANO LA MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA

 Hakuna upendeleo hapa kila mtu yupo na kazi kubwa ya kuchambua na kuhakikisha anapitia vizuri fomu zaidi ya 4,000 za ushiriki wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa chakula
 
 Mmoja ya wa wanachuo akihakikisha mahesabu kama ametoa alama sahihi kabisa wakati wa zoezi hilo la kuchuja na kupitia fomu za washiriki wa shindano la Maisha plus/ Mama shujaa wa Chakula
 Kwa umakini kabisa Kila mmoja anafuatilia na kuangalia fomu kwa umakini wakati wa kuwatafuta wale watakaoingia katika usahili
 Mmoja ya wanachuo akifanya mapitio kwa kusoma kile kilicho andikwa na moja ya fomu za washiriki.
 Baadhi ya wanachuo wakiwa wanasahihisha kwa umakini Fomu za washiriki na kuzipitia ili watende haki wakati wa mchujo huo ambapo Fomu hizo baada ya hapo zinatoka moja kwa moja hadi kwa majaji wakuu ambao hawapo pichani.
 Kazi ikiwa inaendelea kwa umakini

 Mmoja wa wanachuo akitafakari Jambo wakati wa kufanya zoezi la Mchujo
 Kazi zinaendelea
 Mmoja ya wanachuo wa kwanza kulia akimalizia kuhakikisha alama zake katika 'notebook'
***************************
SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA/ MAISHA PLUS
  • Fomu zaidi ya 4,000 za Mama Shujaa Maisha Plus zakusanywa
  • Majaji 9 kusimamia zoezi la kuchaguwa wakulima wanawake 20 na vijana 45
 Zoezi la kuchaguwa washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus limeanza leo  ambapo zaidi ya fomu 4,000 zimekusanywa kutoka kwa washiriki. 

Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akiongea wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo alisema zoezi la kupitia fomu litachukuwa siku nne kuanzia Jumatatu tarehe 3 hadi Alhamisi tarehe 6 Februari 2014. “Majaji walioteuliwa wana kazi kubwa ya kupitia zaidi ya fomu 4,000 ambazo tumekishwazipokea na nyingine bado zinawasili kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu. Baada ya uchambuzi majaji watachaguwa wakulima wanawake 20 pamoja na vijana 45 ambao watashiriki kwenye shindano la mwaka huu. Majaji watasaidia kuchambuwa fomu na vijana 17 waliojitolea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Jinsia.

Jopo la majaji linajumuisha waliobobea kwenye masuala yanayohusu kilimo, ufugaji, usalama wa chakula, sera na utetezi, uchumi, biashara, vyombo vya habari, vijana na maendeleo ya jamii. 

 Majaji ni kama wafuatavyo:
Rose Tesha Meneja Programu ya Maisha Salama shirika la VSO; Masoud Kipanya mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus; Tatu Abdi Juma mshindi wa tatu shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 ; Francis Bonda Mkurugenzi wa kampuni ya DMB na mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus, Edmund Matotay Mtafiti kutoka shirika la Oxfam; Anna Oloshoro mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula mwaka 2011; Carolyn Kandusi mtaalamu wa jinsia kutoka shirika la PINGOS akitokea Loliondo; Zephaniah Mugittu mshauri wa mnyororo wa thamani wa mboga mboga anafanya kazi na shirika la Oxfam akitokea Lushoto, Tanga pamoja na Bernick Kimiro mshindi wa Maisha Plus 2012. 
Washiriki  wa Maisha Plus msimu huu ni vijana wa miaka 21-26 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda wanaogombania kitita cha Fedha za kitanzania Milioni 25.

No comments: