Social Icons

Tuesday 19 August 2014

CHANGAMKIA FURSA MPYA: SERIKALI YATOA FURSA YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WOTE WATAKAOJIUNGA NA MASOMO YA STASHAHADA MAALUM YA UALIMU MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI.



Frank Mvungi_ Maelezo
Serikali  imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya stashahada maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam.
“ Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na stashahada maalum katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo wote watanufaika na mikopo ya elimu ya Juu.”Alisema Mwaisobwa
Akifafanunua, mwaisobwa alisema kuwa lengo la mpango huo ni kusaidia kuondoa tatizo la walimu wa masomo ya sayansi hapa nchini .
Aidha Mwaisobwa alibainisha kuwa jumla ya maombi 58,037 ya mikopo  yalikuwa yamepokelewa hadi kufikia Julai 2014 ambapo maombi 37,689 ni waombaji wa kiume na 19,592 ni waombaji wa kike.
Pia Mwaisobwa alibainisha kuwa majina ya wanafunzi watakaopata mikopo kulingana na udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi  ambayo ni www.heslb.go.tz.na taarifa hiyo itatangazwa katika vyombo vya habari.
Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) inakusanya wastani wa shilingi bilioni 3 kwa mwezi ikiwa ni marejesho ya mikopo iliyokwisha tolewa.


Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

No comments: