Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Wahitimu wa kwanza wa chuo cha ualimu Rungemba Mufindi |
Badhi ya wanafunzi wanaobaki |
Wanafunzi wanaobaki wakiwaaga wenzao kwa kwaya |
Mchungaji Edga Mbadime kulia akiwa na wachungaji wenzake |
Askafu Mkombo na Kigahe kulia |
Wageni waalikwa wakiwa katika mahafali hayo aliyesimama kulia ni Mary Mungai mkurugenzi wa shule za Southern Highlands Mafinga |
Waimbaji wakitumbuiza katika mahafali hayo |
Askofu Mulilege Mkombo |
Mmoja kati ya wadau aliyefanikisha kupata kiwanja |
Bw Exaud Kigahe akihotubia katika mahafali hayo |
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika picha ya pamoja na mhitimu katika mahafali hiyo kutoka kushoto ni Neema Msafiri , Flora Kamaghe na kulia ni Clement Sanga |
Kamati ya mandalizi ya mahafali hiyo |
Viogozi mbali mbali wakiwa katika chuo hicho mara baada ya mahafali |
Mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya chuo cha ualimu Rungemba
wilayani Mufindi mkoani Iringa Bw Exaud Kigahe kutoka wizara ya
viwanda na biashara makao makuu ( wa nane kutoka kulia) akiwa fuatiwa
na mkurugenzi wa chuo hicho Askofu Mulilege Mkombo pamoja na viongozi
wengine wa chuo hicho serikali na chama tawala wakati wakiwa katika
picha ya pamoja na wahitimu hao
...........................................................................................................................................................
Na FGBLOG
KATIKA
kuhakikisha watoto wanaotoka katika familia na uwezo wakiwemo yatima
,kanisa la House of Prayer shield of Faith Cristian Fellowship Church
(HOPS) lenye makao makuu yake mkoani Dar es Salaam limeanzisha chuo cha
ualimu kitakachotoamafunzo ya ualimu kwa gharama nafuu kwa wanafunzi
wake kama njia ya kutekeleza mpango wake wa elimu kwanza.
MKurugenzi
mkuu wa chuo hicho askofu Mulilege Mkombo aliyasema hayo jana
wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika katika
viwanja vya chuo cha Ualimu Rungemba wilaya Mufindi mkoani Iringa .
Alisema
kuwa hatua ya kanisa lake kuanzisha utaratibu wa kujenga chuo
hicho na shule mbai mbali za Sekondari nchini ni kuisaidia serikali
katika kusaidia familia maskini na yatima kuweza kunufaika na
elimu ya gharama nafuu kama njia ya kupunguza ujinga miongoni mwa
jamii ya kitanzania hasa ile isiyo na uwezo wa kusoma katika shule
za sekondari na vyuo ambavyo ada yake ni kubwa .
"
Nilipewa maoni ya kuanzisha chuo hicho na Mungu na Waumini wa
kanisa na HOPS kwa kutambua umuhimu wa elimu waliweza kujitolea
michango yao mbali mbali ya kuanzisha ujenzi wa chuo hicho na
mwaka 2013 chuo hicho kilianzishwa kwa kuwa na wanafunzi 8 pekee ila
kwa sasa ni wanafunzi 43 ndio walioweza kuhitimu kwa mwaka wa kwanza
katika chuo hicho....Yesu Kristo alinielekeza niwahudumie watu katika
Afya na Elimu " alisema askafu Mkombo
Kuwa
moja kati ya kazi kubwa za kanisa hilo ni kuwafanya watu wote
wamjue Mungu na kuwarudisha vijana waliovamiwa na nguvu za giza
katika maisha yanayompendeza Mungu , kuwaponya walioathirika na
utumiaji wa madawa ya kulevya ,kuzuia mauwaji ya kikatili na ugaidi
ili kumrudisha mwanadamu katika utu wa haki na kweli ,kurekebisha
maadili yaliyoporomoka na kuwa huduma hizo zinatolewa kwa watu wote
bila kujali imani zao ,
Askofu
Mkombo alisema katika huduma za kijami lengo la kanisa hilo ni
kuendelea kujenga shule za msingi ,sekondari na vyuo pamoja na
kusaidia kuanzisha Zahanati katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Hata
hivyo alisema kuwa sababu kubwa ya kutoa elimu kwa ada ndogo ni
moja kati ya mkakati wa kanisa hilo katika kuthamini sekta ya elimu na
kuamini kuwa elimu ndio dira peke ya mtanzania huku likiamini kuwa
uwekezaji muhimu ni katika sekta ya elimu na sio mijini pekee bali
hata vijijini ambako siku zote wamekosa fursa
Akielezea
mkakati wa wilaya ya Mufindi katika eneo hilo la chuo cha ualimu
Rungemba alisema ni kuona eneo hilo linajengwa shule ya msingi na
sekondari kwa ajili ya mazoezi kwa wanafunzi wa chuo hicho ambacho
kwa sasa kinatoa mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya cheti ,Diploma peke
japo baadae ni kujenga majengo zaidi kwa ajili ya kuanza kutoa Digrii
ya kwanza na ya pili na kuwa waumini wapo tayari kujenga majengo
hayo ila wanasubiri serikali ya kijiji kuwaongezea eneo la ardhi
zaidi.
Pia
askofu Mkombo alisema kuwa malengo ya kanisa ni kuona kila wilaya na
mkoa wa Tanzania wanajenga shule ,chuo ,zahanati au Hospitali ili
kila mtanzania aweze kupata elimu na huduma za afya kwa gharama nafuu
zaidi .
Alisema
kuwa moja kati ya changamoto katika chuo hicho ni wanachuo badhi
kupata shida ya malazi kutokana na uchache wa mabweni ,pia nyumba
za walimu pia kukosekana kwa Hospitali ama zahanati katika kijiji
hicho cha Rungemba .
Akizungumza
katika mahafali yao mgeni rasmi Bw Exaud kigahe kutoka wizara ya
viwanda mbali ya kupongeza kanisa hilo kwa kuanzisha chuo hicho
katika wilaya ya Mufindi bado alisema akiwa kama mdau wa elimu katika
wilaya ya Mufindi ataungana mkono na jitihada za kanisa hilo katika
kukiendeleza chuo hicho na kuchangia kiasi cha Tsh milioni 1 kwa
ajili ya kusaidia ujenzi wa mabweni .
Bw
Kigahe alisema kuwa yeye ni mkazi wa kijiji cha Nundwe wilaya ya
Mufindi ila amesikitishwa zaidi katika zoezi la uandikishwaji katika
daftari la kudumu la wapiga kura kuona sehemu kubwa ya vijana
ambao wapo chini ya miaka 40 kushindwa kujua kusoma na kuandika
katika wilaya hiyo ya Mufindi na kutaka chuo hicho kuendelea
kutoa furasa zaidi kwa wilaya hiyo .
No comments:
Post a Comment