Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bwana, Juma M. Kanuwa |
CHUO CHA
DIPLOMASIA DAR ES SALAAM, katika kuendeleza wito na wajibu wa kutoa mafunzo ya
muda mfupi na mrefu, mnamo tarehe 31st
March - 4th Aprili 2014
kitafanya kozi fupi ya ITIFAKI NA
MAHUSIANO YA UMMA (PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS) Chuoni Kurasini, Dar es salaam,
Wawezeshaji wa Mafunzo haya ya muda mfupi kawaida huwa ni mabalozi
na wakufunzi waliobobea sana katika mambo ya Diplomasia hivyo kuwapa washiriki
uzoefu na kesi halisi zilizowahi kutokea katika eneo husika la mafunzo ili
kuwajengea uwezo na waweze kwenda kufanyia kazi moja kwa moja mafunzo na
utaalam walioupata.
Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Utafiti,
Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bwana,
Juma M. Kanuwa akilisisitiza
kwamba kutokana na umuhimu wa utaalam wa mambo ya ITIFAKI NA MAHUSIANO YA UMMA
(PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS)
katika sehemu za kazi, mafunzo hayo yatarudiwa tena tarehe 31st March - 4th
Aprili 2014, alisema;
“CHUO CHA
DIPLOMASIA kilifanya mafunzo haya mnamo tarehe
3rd – 7 Februali 2014, lakini kutokana na maombi ya wengi na kwakuwa
mafunzo haya ya PROTOCOL AND
PUBLIC RELATIONS ni muhimu sana
hasa eneo la ‘PROTOCOL’, yatarudiwa tena mnamo tarehe 31st March - 4th Aprili 2014 hapa
hapa Chuo cha Diplomasia ili wale wote walioshindwa kuhudhulia hapo awali
waweze kuja kwa wingi chuoni na kupata mafunzo hayo toka kwa mabalozi na
wataalam waliobobea na wenye uzoefu wa miaka mingi…”
Akaongeza kuwa “..nafasi
zimebaki chache hivyo nawashauri wale wote wanaotaka kushiriki mafunzo haya
waje Chuo cha Diplomasia au wawasiliane na mratibu kwa namba +255713667303 na pia watembelee tovuti ya chuo cha Diplomasia www.cfr.ac.tz kwa maelezo na tangazo la kozi
hii…”
Mafunzo haya ni muedelezo wa mafunzo ya muda mfupi
yaani ‘kozi fupi’ zinazofanywa na CHUO CHA DIPLOMASIA – DAR ES SALAAM, kila
mwezi ambapo kozi mbali mbali zimekuwa zikifanyika, kama Utatuzi wa Migogoro
“CONFLICT RESOLUTION AND MEDIATION” na Usalama wa taarifa ( INFORMATION
SECURITY) iliyofanyika mapema hivi karibuni.
Pia CHUO CHA DIPLOMASIA kinaweza kufanya kozi
kulingana na mahitaji ya taasisi/ wateja na kinakaribisha wadau wote
Kwa maelezo
zaidi wasiliana na Idara ya
Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi,
Mobile: +255713229722, +255713667303
Website: www.cfr.ac.tz
E-mail: lucassoona@yahoo.com
No comments:
Post a Comment