Social Icons

Wednesday 26 August 2015

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) lahitimisha mafunzo ya wiki nane ya Ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

IMG_0595
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini (hawapo pichani) wakati akifunga mafunzo ya wiki nane ya ujasiriamali kwa wanafunzi hao mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Mafunzo hayo yaliendeshwa chini ya mpango wa Cambridge Development Initiative (CDI) ili kuimarisha mafunzo ya maswala ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini.  CDI ni mpango ulioasisiwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini uingereza.  Kulia ni Rais wa CDI, Ravi Solanki.
IMG_0598
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (katikati) akikabidhi hundi ya dola 3000 kwa  wanafunzi wawili kutoka chuo kikuu cha Ardhi walioibuka washindi kwa wazo bora la biashara baada ya mafunzo ya wiki nane ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na NEEC kwa ushirikiano na mpango wa Cambridge Development Initiative (CDI) unaoendeshwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza.  Wengine ni Moses Mtei, mshindi (kushoto); Mkurugenzi wa Ujasiriamali CDI, Bi. Georgia Ware (kulia); na Joel Kissava pia mshindi toka Chuo kikuu Ardhi (wapili kulia).  Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
IMG_0601
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (wa pili kushoto) akikabidhi hundi ya dola 3000 kwa mmoja wa wanafunzi walioibuka washindi kwa wazo bora la biashara baada ya mafunzo ya wiki nane ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na NEEC kwa ushirikiano na mpango wa Cambridge Development Initiative (CDI) unaoendeshwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza. Wengine ni Bhoke Nyaisaba toka UDSM, mshindi (kulia); Mkurugenzi wa Ujasiriamali CDI, Bi. Georgia Ware (wa pili kulia); na mwanafunzi toka UDSM, Vivian Mushi (kushoto). Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

No comments: