Social Icons

Wednesday 29 July 2015

Rais Kikwete atunukiwa shahada ya heshima ya Chuo Kikuu cha Newcastle, Australia

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

n9
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
n10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
n14
Rais Kikwete akimpongeza Bi. Bernadette Mathias ambaye kwa kushirikiana na mpiga piano mumewe Profesa Philip Mathias walitumbuiza kwa wimbo wa “Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote” kwa ufasaha na kusisimua waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
n15
Rais Kikwete na msafara wa wanachuo wakiondoka jukwaa kuu huku wakishangiliwa na waliohudhuria ikiwa ni pamoja na Mama Salma Kikwete na mwana wao Ali Kikwete na ujumbe wa Rais Kikwete kwenye msafara huo.
n11
Sehemu ya umati wa wanachuo na wageni waalikwaa waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
n12
n13
Sehemu ya Watanzania waishio nchini Australia wakipiga makofi wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
n16
Mama Salma Kikwete akimpongeza mume wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
n17
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Newcastle na mkewe Mama Salma Kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
n18
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Ujumbe alioongozana nao mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
n19
Rais Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali Kikwete na Watanzania waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.
n19
n20
n21
Rais Kikwete akipongezwa na raia wa Burundi waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.(PICHA NA IKULU).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle cha nchini Australia.
Sherehe za kumtunuku Rais shahada hiyo zimefanyika leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Newcastle.
Akisoma maelezo ya utangulizi katika hafla hiyo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans amesema Rais Kikwete ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho.
Mkuu huyo wa Chuo amesema Rais Kikwete ametunukiwa shahada hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya duniani si kwa Tanzania tu bali  kwa Dunia nzima kwani mchango wake umetambulika  na  mashirika mbalimbali ya kimataifa yakiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Benki ya Dunia kwa ujumla.
“Tangu kuingia madarakani Rais Kikwete amechangia katika kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu , uchumi na Afya” amesema Bw. Jean na kuongeza kuwa “utawala wake umethibitishia sio Chuo cha Newcastle pekee bali pia kuonesha kanuni ya Msingi kuwa Elimu ni muhimu katika kukuza uchumi, uvumbuzi na katika maendeleo ya jamii” amesisitiza.

Tanzania imekua ikipokea misaada ya elimu kutoka Australia katika nyanja mbalimbali zikiwemo za madini, fedha, habari na tafiti mbalimbali ambazo zimeleta mabadiliko chanya katika jamii na duniani kwa ujumla.
Kwa sasa Watanzania wanne wanachukua masomo ya uzamifu katika masuala ya elimu na siasa.Tayari Watanzania 45 wamemaliza digrii na pia wapo watafiti kutoka Newcastle wanaofanya tafiti zao nchini Tanzania katika masuala ya elimu, afya na uhandisi.
Rais Kikwete ameshukuru na kuelezea jinsi alivyoguswa na tukio hilo ambapo ameushukuru uongozi wa Chuo hicho kwa kutambua mchango wake ambao ameelezea kuwa ameufanya wakati wa kipindi cha uongozi wake kwa moyo, upendo na nia njema kwa wananchi wote wa Tanzania na Dunia kwa ujumla.
“Ilikua nia yangu na wajibu wangu mkubwa kutumia ahadi nilizo waahidi wa Tanzania na hata zaidi ya kile nilicho ahidi na kuelezea kuwa mafanikio haya yote yamechangiwa pia kwa kiasi kikubwa na misingi imara iliyowekwa na viongozi walionitangulia upande wa Tanzania bara na Tanzania Visiwani kwa ujumla”
Katika utawala wake Rais Kikwete ametunukiwa shahada za heshima kutoka vyuo mbalimbali vya Marekani, Canada, China, Uturuki na Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam.
Rais Kikwete pia ametunukiwa tuzo za heshima mbalimbali katika masuala ya Kijamii (United Nations Social Good Award), Afya, Technolojia na Maendeleo (South-South Award for Global Health, Technology and Development) pamoja na Demokrasia (Icon of Democracy Award (Nertherlands)
Rais pia amepata kutunukiwa  na kutambuliwa kwa Mchango wake ambapo alitunukiwa nishani kadhaa zikiwemo;
1.(Most Excellent Order of the Peral of Africa) ambayo ni nishani ya juu nchini Uganda.
2.The order of the Green Crescent of the Comoros (Comoros)
3.Order of Abdulazizi Al Saud (Saudi Arabia)
4.Order of excellence (Jamaica)
5. Order of Oman (Oman)
6. AAI African National Achievement Award
7. U.S. Doctors for Africa Award
8. Good Governance in Africa  2015
Sherehe hiyo imehudhuriwa na Mstahiki Meya  wa mji wa Newcastle, Mama Nuatali Nelmes, walimu na wakufunzi wa Chuo cha Newcastle, wanafunzi wa Kitanzania na familia zao pamoja na Watanzania kadhaa wanaoishi na kufanya kazi katika mji wa Newcastle.
Rais Kikwete amekamilisha ziara yake ya Kiserikali ya siku nne nchini Australia na anatarajia kuelekea Dar-es Salaam tarehe 30 Julai, 2015
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Newcastle-Australia
29 Julai, 2015

No comments: