Social Icons

Monday 24 November 2014

HOT NEWS: ASKARI MTUHUMIWAWA MAUAJI YA MWANAFUNZI WA TEKU AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA.

ASKARImmoja kati ya watatu waliokuwa wakituhumiwa kwa mauaji kwa aliyekuwa mwanafunziwa Chuo kikuu TEKU, amehukumiwa kunyongwa hadi kufa huku wenzie wakiachiwahuru.
Hukumuhiyo ilitolewa katika Mahakama kuu kanda ya Mbeya na Jaji Rose Temba baada yakuridhishwa na ushahidi wa pande zote mbili uliotolewa mahakamani hapo kwanyakati tofauti.
Mwendeshamashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa akisaidiwa na Catherine Paul aliwatajawashtakiwa kuwa aliyehukumiwa ni Askari polisi F5842DC Maduhu na walioachiwa ni pamoja na F 7769 DC Shaban na WP 6545 DC Neema baada yakuwakuta hawana hatia.
Mtuhumiwahuyo amepatikana na kosa hilo kwa mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu chaTeofilo Kisanji(TEKU) Daniel Mwakyusa aliyekuwa mwaka wa kwanza wa masomo mwaka2012.
Hukumuhiyo ya imetolewa na jaji Rose Temba baada ya kuridhishwa na ushahidiuliotolewa na pande zote mbili. 
Awali ilielezwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali Archiles Mulisa akisaidiwa naCatherine Paul kuwa washitakiwa wenyekesi namba 16 ya mwaka 2013 walifanya mauaji ya kukusudia mnamo Februari 14mwaka 2012 kinyume cha kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kamailivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Wakili Mulisa alisema washitakiwa hao kwa pamojawalihusika na mauaji ya Daniel Mwakyusa baada ya kumpiga marehemu huyo kwakutumia silaha inayodhaniwa kuwa ni bunduki nje ya ukumbi wastarehe ujulikanao Univesal uliopo Uyole jijini Mbeya.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo,jajiTemba alisema anawaachia huru mshitakiwa namba mbili DC Shaban ambaye alikuwadereva wa gari ya polisi kwakuwa ushahidi uliotolewa unadhihirisha kuwa alibakindani ya gari akimsubiri mshitakiwa namba moja aliyeshuka na kuingia kwenye bar hiyo.
Kwa upande wa mshitakiwa namba tatuDC Neema,Jaji Temba alisema aliridhishwa na mshitakiwa huyo kutohusika namauaji kwakuwa siku ya tukio alikuwa akijisikia vibaya hivyo alilazimika kubakina dereva kwenye gari.
Jaji Temba alisema mshitakiwa nambamoja DC Maduhu anahusika moja kwa moja na mauaji hayo kutokana na ushahidi wakimazingira kwani yeye ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho kuondoka na marehemu eneola tukio na kumpeleka kwenye gari.
Alisema sababu ya pili,ushahidiulionesha kuwa silaha yake pekee ndiyo iliyotumika tofauti na za askari wenginekwakuwa risasi tatu zilionekana kupungua kati ya zile alizokabidhiwa sambambana ushahidi wa maganda matatu ya risasi yaliokotwa eneo la tukio.
Aidha,Jaji Temba alisema sababu yatatu ni kuwa ushahidi uliotolewa unaonesha kuwa mshitakiwa huyo alikuwa wamwisho kurejesha silaha hivyo kuhusishwa moja kwa moja na mauaji hayo.
Alisema kutokana na sabvabu hizomahakama inamtia hatiani kwa kuua kwa kukusudia hivyo mshitakiwa DC Maduhuamehukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Awali ilidaiwa kuwa siku ya tukioilikuwa siku ya wapendanao(Valentine Day) ambapo mtuhumiwa akiwa doria naaskari wenzie alimkuta marehemu akiwa kwenye eneo la starehe na mwanamke anayesadikiwakuwa alikuwa pia na mahusiano na askari huyo.

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

No comments: