Social Icons

Saturday 26 July 2014

TAMASHA LA NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015‏



  Mwakilishi wa Wakuu wa Vyuo ,Mwl. Mwalimu Kasilima Kasi,(kushoto), kutoka Chuo cha DAR ES SALAAM CITY COLLEGE (DACICO TANZANIA), akifafanuan jambo kuhusina na MICHEZO hiyo kwenye vyuo vya Elimu ya kati.wengine Katika picha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, Mr. Mpalule Shaaban, Mwakilishio wa Serikali za Wanafunzi Vyuoni, Mr. Stephano Stephano , kutoka chuo cha C.B,E, Mratibu wa Tamasha hilo Bi. Magreth Kilawe, Afisa mahusiano wa kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, Bi. Rozina Mcomvu, Mwakilishi wa Ikondolelo Lodge, Wadhamini Wadogo, Jane Charles na Mwakilishi wa Michezo ya Wanawake(Modoling & Beuty) Bi. Vanessa Wlliam kutoka chuo cha Eden Hill College. hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Idara Habari Maelezo.(Picha kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).
Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi Vyuoni, Mr. Stepano Stephano, wa pili kushoto, akifafanua jambo kuhusiana na Michezo ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, itakayohusisha vyuo mbali mbali hapa nchini kushiriki michezo.wengione kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, Mh. Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha Bi. Magreth Kilawe na Afisa mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi. Rozina Mchomvu.mazungumzo hayo yamefanyika ukumbi wa Idara habari Maelezo, Dar es Salaam jana.
  Mratibu wa Tamasha la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015, Bi, Magreth Kilawe,(kati), akifafanua  kwa waandishi wa habari, kuhusiana na Tamasha la Vyuo vya Elimu ya Kati na Vilivyopata Usajili wa NACTE, mikoa yote ya Tanzania kwa kushirikisha michezo mbali mbali, hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Idara habari Maelezo, kushoto ni Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano na Afisa Uhusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi, Rosina Mchomvu.
 Mratibu wa Tamasha la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015, Bi, Magreth Kilawe,(kati), akifafanua  kwa waandishi wa habari jambo, kuhusiana na Tamasha la Vyuo vya Elimu ya Kati na Vilivyopata Usajili wa NACTE, mikoa yote ya Tanzania kuhusu kushiriki michezo mbali mbali, hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Idara habari Maelezo, kushoto ni Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano na Afisa Uhusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi, Rosina Mchomvu,(kulia) wa kwanza aliyesimama ni mwenyekiti wa Kamati ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, Mh. Mpalule Shaaban na Mwakilishi wa Mdhamini Mdogo kutoka MLONGE MORINGA.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini, kuhusiana na Taarifa za Tamasha kubwa la Vyuo vya Elimu ya Kati chini ya NACTE TANZANIA, ambalo linashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo SOKA, mchezo ambao unapendwa na watu wengi, Netball, Basketball, Voleyball, Handball, kuimba, Muziki, Mijadala (Debate) na Urembo wenye tija zinazokidhi  taifa katika Maharifa(Akili) na si mavazi.(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania)
 Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe,(kati), akitoa ufafanuzi kwa  waandishi wa habari wa Sahara Media Group,  kuhusiana na Tamasha la Vyuo vya Elimu ya Kati na Vilivyopata Usajili wa NACTE, Michezo inayotarajiwa kuanza kwenye vyuo hivyo mapema mwezi wa kumi na moja mwaka huu, ambapo Vyuo vimetakiwa kukamilisha zoezi la usajili wa Wanamichezo wao mapema.

****************************
 
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
PRESS RELEASE
                                                                       
NACTE INTER - COLLEGE TANZANIA BONANZA 2014/15.
(BALOZI WA DEMOKRASIA TANZANIA).
                                                                                                                                24/7/2014
HABARI za wakati huu,
Waandishi wa habari wote, wakuu wa vyuo na viongozi wa Serikali za wanafunzi wa vyuo shiriki, wadhamini, Karibuni sana.
Leo ni siku rasmi, ya kutangaza kuanza kwa mchakato mzima wa maandalizi ya mashindano ya NACTE Inter-College Tanzania Bonanza 2014/15, ambayo kwa mara ya kwanza yataanza kuonesha sura na muonekano mpya katika Sekta ya Elimu kwa ngazi ya Vyuo vya Kati.
 
Bonanza hili limepangwa kufanyika 21-23/11/2014 katika viwanja vilivyopendekezwa ikiwa ni pamoja na The Mwalimu Nyerere Memoria Academy,(Kigamboni) Chuo Kikuu Dar es Salaam, Leaders Club, TCC Sigara (Chang’ombe, na viwanja vya Shule ya Sekondari Kibaha Katika michezo mbali mbali .
Ndugu wandishi, tamasha hili lipewa kibali na baraza la elimu ya ufundi yaani NACTE katika barua yao ya tarehe 21/6/2014 yenye kumb No. NACTE/EB/64/650/Vol.1/2 ambayo inairuhusu kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania kwa kushirikiana na Tone Multimedia Group, kuandaa na kuwa mwenyeji wa Tamasha la NACTE Inter College Tanzania. 
 
Nichukue fursa hii kuishukuru Serikali kwa kukubali kuipa heshima kubwa kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, ubavu wa kuandaa tamasha hili, lakini pia tunaiomba Serikali kuhamasisha wadau kujitokeza kusaidia vifaa vya michezo hii.
kwa kushirikiana na  vyombo vya habari hapa nchini na vyuo husika, Wadhamini ambao hao ni wadau namba moja, wawezeshaji   tutaifanaya kwa ustadi na kwa makini mkubwa ili mwaka ujao kuwe na msisimko zaidi,
 ikumbukwe kuwa michezo  hii inafanyika kwa mara ya kwanza hapa Tanzania. Itakuwa ni fursa kwa wanafunzi wa vyuo vya kati, kwa nafasi zao kuendeleza vipaji walivyonavyo,  kwa kuwa,  kwa muda mrefu hawajapata nafasi kama hii,  ya kushiriki katika michezo pindi wanapoingia kwenye vyuo,  baada ya masomo ya Elimu za Sekondari.
Ndugu waandishi, Michezo, kama tunavyofahamu ndiyo pekee inayoweza kutoa fursa kwa vijana,  kupata afya nzuri, ajira katika michezo, pamoja na nafasi ya kuitangaza Tanzania,
 kupitia Michezo vijana upata fursa ya kusikilizwa na kufikisha mawazo yao, na mambo mbalimbali yanayohusu afya na maendeleo yao ikiwemo Ujasiriamali, Elimu ya UKIMWI na mengine mengi yakiwemo kutambua nafasi ya kijana katika kutunza na kulinda amani ya Nchi yetu.
Pamoja na kuwa na nchi yenye amani; michezo pia utoa fursa ya vijana kujiendeleza kiujasiriamali,  lakini pia kwa kupitia tamasha hili inaweza kuwa fursa ya makampuni, wahisani, wadau, kukamilisha ndoto zao, katika kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wanaohitimu vyuo vya kati.
tumieni  kalamu zenu, Mic, Kamera, kuhamasisha Michezo hii na Wadau kujitokeza kusaidia michezo hii ya vyuo vilivyo pata usajili wa NACTE.
wito unatolewa kwa vyuo, kuthibitisha ushiriki wao mapema, kabla ya tarehe 15/8/2014, Michezo hii ni kwa vyuo vyote vya NACTE Tanzania, baada ya Dar es salaam, itafuata Mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na Zanzibar Fomu zinapatikana kwenye Tovuti,
Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, ilianzishwa Mwaka 2009, na kupata Usajili wa kudumu wa Makampuni unaotambuliwa Kisheria wa Act, 2002 No. 74413 mwaka 2010, na TIN No: 109-267-554. Kampuni hii ambayo kwa ujumla kama lilivyo jina lake, (Miss Demokrasia Tanzania) ina malengo mengi, ikiwa na pamoja na kusaidia jamii hususani vijana wa kike, ambao muda mwingi wamekuwa wakishindwa kufikia malengo kutokana na ukosefu wa miundo mbinu ya kujikomboa kielimu, Utamaduni na Michezo, Ajira,  kwani wengi wao wameoonewa na kunyimwa haki zao.
kampuni hii inalinda na kutetea haki za watu wote ikiwa ni pamoja na kuwapa changamoto Viongozi mbali mbali wa serekali na Taasisi binafsi dhidi ya utendaji wao wa kazi na majukumu ili kuongeza na kuboresha ufanisi wao wa kazi kwa wananchi, imejikita sana kwenye masuala ya Intertainment Michezo, Maonesho, Burudani, Mikutano, Mijadala (Debate), Elimu kwa Jamii, na Urembo (Modal) kwa namna ya kipekee.
Mwisho: kabisa nirudie tena kuishukuru Serikali na Uongozi wa NACTE kwa kuweka na kukubali mpango huu wa Michezo kwenye vyuo vya kati. Tutumie nafasi hii, kuwakaribisha wahisani na Wadhamini wote, kushiriki kikamili na kwa namna yoyote ile ili kufanikisha Tamasha hili la NACTE – INTER – COLLEGE - TANZANIA – 2014 / 2015.
Niwashukuru wadhamini walioanza kujitokeza, IKONDOLELO HOTELI Lodge wanaopatikana Kibamba CCM, MLONGE MORINGA, na Tone on line Radio T-z.
Baada ya kusema hayo. Asanteni Wote kwa kunisikiliza.  niwape nafasi wawakilishi wa Vyuo, na wadhamini waseme japo waliyo nayo…
Magreth Kilawe                                                                                             Rosina Mchomvu                      
Afisa Masoko                                                                                                   Afisa Habari
 
Kwa Mawasiliano Zaidi:
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment C.o LTD.
Plot No.
S.L.P 8017, Dar Es Salaam,
Simu: +255-767-869-133
+255-765-056-399



Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

No comments: