Social Icons

Thursday 24 July 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) Imeandaa Kongamano la kujadili mchakato wa kupata Katiba mpya.

Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), Imeandaa Kongamano la kujadili mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kongamano hilo litafanyika tarehe 27 Julai 2014 siku ya Jumapili kuanzia saa 8 mchana ndani ya ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star TV
Mada kuu ya kongamano hilo ni, Tujadili na Kutafakari Mchakato wa Katiba Mpya kwa Manufaa ya Taifa Letu”.
Watoa Mada katika kongamano hilo ni Prof. Y. Msanjila na Dkt. Kitila Mkumbo
Tunapenda kuchukua fursa hii kwa heshima kubwa kuwakaribisha wananchi wote ili wawe miongoni mwa watu watakaotoa mchango wao mkubwa katika mchakato wa kuleta maridhiano ya kitaifa kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya ya taifa letu la Tanzania.
Tutanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushiriki wako kwenye kongamano hili.
Imetolewa na
Bw. Faraja Kristomus.
(Katibu – UDASA)
 
0787 52 53 96 / 0717 086 135


Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

No comments: