Social Icons

Wednesday 18 June 2014

MPYA : SOMA MAJINA YA WALE WOTE WALIOITWA KWENYE USAILI AWAMU YA PILI UHAMIAJI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wasailiwa 1,281 kati ya 6,115 waliofanya usaili wa kwanza tarehe 13 Juni, 2014 jijini Dar es Salam kuomba nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji (Assistant Inspector of Immigration) wanatarajiwa kuingia duru ya pili na ya mwisho ya usaili huo baada ya kufanikiwa kufaulu usaili wa kwanza.

Usaili huu ambao utafanyika kwa awamu utaanza tarehe 23 Juni hadi 03 Julai, 2014 na utafanyikia katika Bwalo la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1.30 asubuhi.

Tofauti na usaili wa kwanza ambao ulikuwa wa kuandika na ulihusisha maswali ya hesabu na ufahamu wa jumla, usaili wa awamu ya pili utakuwa wa maswali ya ana kwa ana ambao utahusisha kupima uwezo wa msailiwa kujieleza na kufafanua mambo.

Kuchaguliwa kwa wasailiwa hawa kulifanyika baada ya kusahihisha majibu yao na majina kuingizwa katika mfumo wa kimtandao ambao ulisaidia kuchagua wasailiwa waliopata alama hamsini na kuendelea.

Majina ya wasailiwa hawa yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, www.moha.go.tz  na ya Idara ya Uhamiaji, www.uhamiaji.go.tz na watatakiwa kuja na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa, vya shule na picha mbili za pasipoti.
BOFYA LINK HIYO HAPO CHINI KUSOMA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI

Awali, kiasi cha wasailiwa 10,801 waliitwa kwa ajili ya usaili wa kwanza
baada ya kupokea maombi yao, lakini waliohudhuria ni 6,115 na kati yao ndio walipatikana 1,281 ambao watasailiwa ili kupata watakaojaza nafasi sabini (70) za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji katika Idara ya Uhamiaji.

Sgn Isaac J. Nantanga
0754 484286
MSEMAJI,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments: