Social Icons

Saturday 31 August 2013

SERIKALI KUJENGA CHUO KIKUBWA CHA MAFUNZO YA UFUGAJI NYUKI NCHINI


NASISITIZA TUTAJENGA CHUO KIKUBWA HAPA CHUONI TABORAWaziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akiwasisitizia wahitimu na wageni (hawako pichani) waliofika katika mahafali ya kwanza na ya pili ya Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora kuwa serikali lazima ijenge Chuo KIkubwa Cha Ufugaji Nyuki Tabora.
…………………
Na Tulizo Kilaga, Tabora
SERIKALI imeahidi kujenga chuo kikubwa cha mafunzo ya ufugaji nyuki katika eneo la Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki mkoani Tabora ili kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya kwanza Barani Afrika katika uzalishaji wa mazao yatokanayo na nyuki.
Ahadi hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda aliyekuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya kwanza na ya pili ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora alipokuwa akiwahutubia wahitimu kabla ya kuwatunuku vyeti na zawadi.
Mhe. Pinda alisema pamoja na mapungufu ya chuo hicho yaliyotokana na tabia ya kuhamisha mafunzo yake mara kwa mara kwenda kwenye vyuo mbalimbali vya Wizara ya Maliasili na utalii nchini, chuo kina umuhimu mkubwa kutokana na kuwa ni chuo pekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
“Siku za nyuma chuo kiliweza kupata watu kutoka nchi za nje kuja kujifunza, hivyo serikali haiwezi kukiacha solemba! Kama tumeweza kujenga Chuo kikubwa cha Serikali za Mitaa, Hombolo kinachotufanya tushindwe kujenga chuo  kikubwa hivi ni nini? Kwamba hatuoni thamani yake? Si kweli, miaka kumi ijayo thamani yake itaonekana tu,” alisema Mhe. Waziri Mkuu.
Aliongeza kuwa, tatizo la kutoendelezwa kwa chuo hicho wakati mwingine kunatokana na viongozi kutojua kinachoendelea, hivyo aliomba uongozi kuwakilisha mpango mkakati wake ili serikali iweze kuipembua na kuona wapi pakuanzia

No comments: