Social Icons

Saturday, 22 September 2012

KILIO CHA WANAFUNZI WANAOJIUNGA NA CHUO KIKUU CHA DODOMA



 


Salaam,
tafadhali tusaidie sisi wanafunzi wa Mwaka wa kwanza tuliochaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambao hadi leo hatujapata Admission Letters zetu hadi hii leo na Baadhi tunatakiwa tuzitumie hizo kuombea ruhusa makazini hasa wafanyakazi wa Serikali, je tunafanyaje na UDOM waliweka tangazo hili hapa chini wiki ya ya pili na zaidi sasa.

Tunashangaa barua hazitoki ilhali TCU wao wamesha toa majina ya watakao jiunga hapo na hata Bodi ya Mikopo nayo imetoa majina.

Tunaomba tupatiwe barua zetu maana Chuo karibia kinafunguliwa kwa sisi wa 1styear.

Admission Letters For First Year Students for Academic Year 2012/2013

Announcement to All first year Students for Acadmic Year 2012/2013
Be Informed that If your Name Do not appear on the List of Selected Students Published on UDOM website, you will not be able to Download your Admission Letter. For Second batch and Equivalent Students the list of Selected Students will be publised at Mid the Next Week.
For those who their Names Appears on the List, The admission Letters are Downloaded on the following Link, Please make sure you Read the Instructions.

NAWASILISHA


Friday, 21 September 2012

HAYA NDIYO MAJINA YA WANAFUNZI WALIO CHAGULIWA KUJIUNGA NA ELIMU YA JUU 2012/2013, PIA TAZAMA MAJINA YA WALIO PATA MKOPO PAMOJA NA SCHOLARSHIPS HUKO MOZAMBIQUE !


SELECTED APPLICANTS FOR THE 2012/2013 ADMISSIONS

The Tanzania Commission for Universities (TCU) in Collaboration with the National Council for Technical Education (NACTE) is announcing the names of Applicants who were seleted into various programs for the 2012/2013 Admissions. However, the list of  some applicants who were selected into various programs but obtained no loan, applicants who were returned by some institutions, and selected applicants who asked for transfer, will be announced before 21 September 2012
 
To view selected applicants with Loans, please click here...

To view selected applicants through Mozambique Scholarships, please click here...

To view selected applicants with Loans but subject to verification with HESLB (Previous Lonee), please click here ... 
 

WANAFUNZI WALIOPATA MIKOPO 2012/2013 BOFYA HAPA

KWA MAELEZO ZAIDI INGIA http://www.tcu.go.tz

Monday, 17 September 2012

Wasiwasi wa mikopo wakumba wanafunzi vyuo vikuu





Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini, wako hatarini kuchelewa kupata fedha za mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutokana na mchakato wa kutoa mikopo hiyo kuchelewa kuanza.

Hali hiyo inatokana na vyuo hivyo kuanza kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu na mwanzoni mwa mwezi ujao.

 Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE umebaini kuwa wanafunzi katika vyuo hivyo walioomba mikopo toka HESLB, bado hawajaanza kupata hatua ambayo imeanza kuwapa shaka kama wataripoti vyuoni kwa wakati kutokana na kutegemea fedha za mikopo kwa ajili ya ada ya masomo na mahitaji mengine.

Kutokana na ucheleweshaji wa mikopo hiyo, gazeti hili lilishudia wanafunzi kadhaa ambao wamedahiliwa kujiunga vyuo vya elimu ya juu mwaka huu, wakimiminika katika ofisi za HESLB makao makuu jijini Dar es Salaam kuulizia hatma ya mikopo waliyoomba.

“Unavyoniona hapa ni wiki ya tatu nimekuwa nikija hapa ofisi za Bodi ya Mikopo kuulizia kama mikopo imeanza kutolewa, lakini tunaelezwa tuendelee kusubiri wakati vyuo vimekaribia kufunguliwa,” alisema mwanafunzi mmoja aliyetoka Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.

Hata hivyo, Afisa mmoja wa HESLB, aliyejitambulisha kwa jina moja la Venelanda, alisema mchakato wa kuandaa mikopo ya wanafunzi bado unaendelea na kwamba zoezi hilo linachukua muda kidogo kutokana na mikopo hadi kukamilika kwake hupitia maeneo mengi.

Venelanda ambaye hata hivyo, hakutoa jibu la moja kwa moja kama mikopo kwa wanafunzi hao itaanza kutolewa lini, alisema HESLB itahakikisha mikopo hiyo inatolewa kwa wanafunzi hao kabla ya kufunguliwa vyuo hivyo.

Mkuu wa Idara ya Habari Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, alipoulizwa na gazeti hili kama fedha za mikopo kwa wanafunzi wa  elimu ya juu zimeshapelekwa HESLB, alisema suala hilo waulizwe Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

“Bajeti ikishapitishwa bungeni, kinachobakia ni kwa wizara husika kushughulikia mipango yake, hivyo hata suala la fedha za mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu  wenye majibu ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,” alisema Mduma.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo, alipoulizwa na NIPASHE, alisema kimsingi mikopo bado haijaanza kutolewa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na kufafanua kuwa kuanzia wiki hii wizara yake itaangalia uwezekano wa kushughulikia suala hilo ili wahusika wapewe mikopo hiyo.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Bhokombe Itembe, alisema wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanatarajia kuripoti chuoni hapo Oktoba Mosi, mwaka huu.

Alisema wiki iliyopita uongozi wa chuo na Daruso, walitaka kupanga vyumba katika hosteli kwa ajili ya wanafunzi, lakini zoezi hilo lilishindikana kwa sababu bado haijafahamika idadi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza watakaoripoti chuoni hapo.

Itembe alisema tatizo la kuchelewa kwa mikopo linatokana na sababu kadhaa, ikiwemo kutokuwepo kwa ushirikiano kati ya HESLB na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

“Mwanafunzi anapodahiliwa bila TCU kumuamulia ataenda chuo gani, huwezi kwenda na wakati huo huo bila HESLB kukupatia mkopo, vile vile huwezi kwenda chuoni,” alisema Itembe.

Rais wa Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha IFM, Michael Chazy, alisema chuo hicho kitafunguliwa Oktoba 8, mwaka huu na kwamba hadi sasa bado wanafunzi wanaoendelea na wale wa mwaka wa kwanza hawajaanza kupatiwa mikopo.

Naye Rais wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Paul Yunge, alisema suala la mikopo katika chuo lina utata hasa kwa wanafunzi wanaoanza mwaka wa kwanza ambapo baadhi yao wamejaza fomu vibaya na hivyo taasisi husika zinashughulikia tatizo hilo.

Rais wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Amos Chakushemeire, alisema utoaji wa mikopo hauridhishi kabisa katika chuo hicho ambapo wanafunzi walioanza muhula Julai, mwaka huu, wamelipwa robo ya mkopo wakati kiasi kingine cha mkopo hawajalipwa hadi sasa, hali ambayo imesababisha ukata mkubwa kwa wanafunzi.

“Chuo chetu ni tofauti na vingine, kina mihula mitatu, wanafunzi walioanza muhula wa Julai hawajalipwa sehemu nyingine,. Hivi karibuni uongozi wa chuo ulilazimika kuwakopesha Sh. 50,000 wanachuo hao ili kuwatuliza wasigome,” alisema Chakushemeire.

Rais wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Frank Nkinda, alisema mikopo ni changamoto kubwa katika chuo hicho ambapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza hawajapata mikopo hadi sasa.

Alisema kutokana na hali hiyo, hivi karibu Mwenyekiti wa HESLB alifika chuoni hapo kuzungumza na uongozi, serikali ya wanafunzi na wanachuo ambapo alitoa ahadi kutoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika mwaka huu wa 2012/2013.

Mwaka jana serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza utaratibu mpya wa utoaji wa mikopo ambapo badala ya fedha hizo kutolewa kwa waombaji na HESLB, sasa fedha hizo zinapelekwa vyuoni ambako menejimenti za vyuo zinawajibika kuzisimamia na kuwapa waombaji.

Hatua hiyo ilifikiwa ili kurahisisha mchakato wa kuwapatia fedha waombaji na pia kuepusha usumbufu kwa HESLB kutokana na wanafunzi kutoka vyuoni kuvamia ofisi hizo kwa lengo la kushinikiza wapewe fedha.

Taarifa iliyotolewa na HESLB na TCU Agosti 10 na 12, mwaka huu ilieleza kuwa zaidi ya wanafunzi 3,074 walioomba mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2012/13, wameenguliwa katika maombi yao kutokana na dosari mbalimbali.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa HESLB pekee iliorodhesha zaidi ya wanafunzi 2,649 ambao ilibaini kuwa na mapungufu kadhaa katika maombi yao ya kupewa mikopo.

Miongoni mwa makosa ama dosari ambazo HESLB ilizibaini kwa walioenguliwa ni pamoja na kukosekana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa muombaji, sahihi ya mdhamini/muombaji, kukosekana kwa picha ndogo ya muombaji/mdhamini, kukosekana kwa sahihi za viongozi wa serikali za mitaa/vijiji kwa waombaji na nyaraka nyingine muhimu kwa waombaji.

Kwa upande wake TCU, iliwaengua jumla ya waombaji 425 kwa dosari na makosa mbalimbali.

Miongoni mwa dosari ambazo zilitajwa na TCU ni pamoja na baadhi yao kukosea namba za vyeti vya masomo kwa vidato vya nne na tano, miaka ya kumaliza masomo, mawasiliano sahihi kwa muombaji pamoja na uchaguzi wa masomo.

Hata hivyo, taasisi hizo mbili zimetoa muda kwa walioenguliwa sasa kutokana na dosari hizo kurekebisha na kutuma tena maombi yao kupitia mitandao kwa mujibu wa maelekezo waliyotoa.

Kwa mwaka huu wa fedha 2012/13, serikali imeiongezea fedha HESLB kwa kuitengea Sh. bilioni 326 kwa wanafunzi 98,772.

Mwaka jana, serikali iliitengea HESLB Sh. 91,722,783,264  kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Ucheleweshaji wa fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu umekuwa ukisababisha wafanye migomo, vurugu na maandamano mara kwa mara kushinikiza walipwe.




 NA THOBIAS MWANAKATWE
CHANZO: NIPASHE

Sunday, 16 September 2012

MKUTANO WA WANAFUNZI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NOVEMBA 14



Mkurugenzi wa Mauzo wa Shirika la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini (AIESEC), Frank Mushi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandhi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mkutano utakaofanyika Nov.14-18. Kushoto ni Kiongozi wa maandalizi ya mkutano huo, Gwamaka Mwabuka na Rais wa AIESEC, Echo Wong
----
Na Shehe Semtawa


SHIRIKA la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini (AIESEC), litakuwa mwenyeji wa mkutano wa vijana zaidi ya 400 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaozungumzia ushiriki wa vijana katika jumuiya hiyo.


Akizungumza na wandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es salaam leo, Msemaji wa Shirika hilo, Frank Mushi alisema mkutano huo utakuwa wa siku tano, kuanzia Novemba 14 hadi 18 mwaka huu.


Alisema mkutano huo unalengo la kuwajengea uwezo wa kujiwezesha katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali katika jumuiya hiyo.


Mushi alisema mkutano huo ni wa sita tangu kuanzishwa shirika hilo miaka 13 iliyopita ambapo zaidi ya wanafunzi 35,000 wamenufaika kwa kujiajiri katika nyanja mbalimbali za kijasiriamali nchini.


“Katika mkutano wetu huo tutajadili namana ya kuzuia mchafuko vile vita ya dunia iliyopita, huko nyma, hivyo kukutana kwetu sisi vijana tutaweza kujifunza mambo mengi ya msingi na maedeleo katika nchi zetu”alisema Mushi.


Frank alizitaja nchi ambazo zitashiriki katika mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Saam ni pamoja na Kenye, Uganda, Rwanda, Burundi na wenyeji Tanzania.

Friday, 14 September 2012

WANAFUNZI USTAWI WATUNUKIWA SASA WAJUA ALAMA ZA NYAKATI



Wanafunzi
wa chuo cha Ustawi wa jamii waliohitimu mafunzo ya Lugha za alama za
Viziwi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi Kaimu Kamishna wa
Ustawi wa Jamii, Jeanne K. Ndyetabura  (aliyekaa mstari wa mbele
katikati akiwa na vazi la suti). Jumla ya Wanafunzi 134 walihitimu
mafunzo hayo kwa mara ya kwanza tangu chuo hicho kianzishwe hapa nchini. Meza kuu ambapo kutoka kulia ni
Dk. Theresia Kaijage (Kamishna mstaafu wa Ustawi wa Jamii), Mlwande
Madihi (Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Ustawi wa Jamii), Abdallah
Nyange (Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi na muhitimu wa mafunzo ya
lugha za alama), Jeanne K. Ndyetabura (Kaimu Kamishna wa Ustawi wa
Jamii), Dk. Naftari Ng’ondi (Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii), Lupi
Mwaisaka Magwanya (CHAVITA) na Paulo Wadugu (Mwalimu wa alama za lugha)
Mwenyekiti
wa wanafunzi waliohitimu, Abdallah Nyange (kushoto) akiwasiliana na
Mwalimu wake Paulo Wadugu (kulia) kwa njia za alama za nyakati.
 
Mwenyekiti
wa wanafunzi waliohitimu, Abdallah Nyange (kushoto) akiwasiliana na
Mwalimu wake Paulo Wadugu (kulia) kwa njia za alama za nyakati.

Tuesday, 11 September 2012

RAIS KIKWETE AFUNGUA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI,KUNDUCHI JIJINI DAR


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha UIinzi (National Defence College) leo Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala na kushoto kabisa ni aBalozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Younqing.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala leo Septemba 10, 2012 baada ya kumkabidhi mfano wa funguo kama ishara ya kufungua rasmi chuo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma akipozi na wanachuo wa kozi ya kwanza ya bmwaka mmoja katika Chuo cha UIinzi (National Defence College) alichofungua rasmi leo Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam.
PICHA NA IKULU.

Sunday, 9 September 2012

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU YATAFUNA FEDHA ZA WANAFUNZI HUU NI MFANO MMOJA WAPO



Financial
statement inayoonyesha kiwango anachodaiwa wakati fedha hizo
hazikulipwa na mwanafunzi huyu bado anadaiwa na chuo na kimeshikilia
vyeti vyake
Barua
ambayo chuo kiliandika kuonyesha kuwa fedha zilirudishwa bodi baada
ya kuwa hazikusainiwa na wanafunzi.na kuwa fedha ya mwaka wa pili
haikulipwa kabisa na bodi ya mikopo
Baada
ya kufuatilia suala lake,alilifikisha hadi wizara ya elimu,na wizara
ikawaandikia bodi kutaka kujua ukweli wa madai haya,Barua hii
haikujibiwa
Baada ya bodi kutojibu barua ya kwanza,wizara iliandika tena kuulizia suala hilo,Hadi sasa bado bodi haijajibu kitu.

Bodi
ya mikopo,inalalamikiwa kutafuna fedha za mwanafunzi MWESIGA
CHRISTIAN MICHAEL aliyehititimu DUCE mwaka 2011.Bodi inaonekana
hawakulipa ada yake ya mwaka wa kwanza na wa pili,bali walilipa ya
mwaka wa tatu pekee.
Alipokuwa
akifuatilia akiwa bado chuoni alikuwa akiambiwa hakuna tatizo na ada
zote zitalipwa.Bali amejikuta akidaiwa na chuo ada ya miaka 2 zaidi ya
milion 2 na chuo kimezuia vyeti vyake.
Bodi
ya mikopo ambayo aliingia nayo mkataba sasa inasema haimtambui na
bajeti yake haipo tena.Hata hivyo uchunguzi wetu umegundua kuwa kuna
udanganyifu mkubwa kwa upande wa bodi kwani financial statement
waliyotoa inaonyesha amelipiwa ada.
Upekuzi
wa Mtandao huu megundua kuwa bodi,ama watumishi wake walighushi kwa
makusudi na kubadili majina ya mnufaika na kulipa mtu hewa kwa miaka
2,ila wakalipa mtu stahiki mwaka wa tatu pekee
.
Ajabu
hata hivyo,Mwesiga Christian Michael,hakunufaika na fedha hizo,bado
anadaiwa na chuo na vyeti vyake vimezuiwa.Kinachokera zaidi ni kuwa
inaonekana anadaiwa zaidi ya milioni 7 wakati hazikulipwa fedha hizo.

Ni wazi kuna udanganyifu na au wizi kwenye bodi ya mikopo.

Mtandao huu umeshindwa kujua ni vipi bodi imekaidi kujibu barua za
wizara mara mbili juu ya madai ya Mwesiga.Tunadhani wenye kuhusika
watafutwe na mamlaka husika ili wawajibike kwa wizi walioutenda.Hadi
sasa Mwesiga hajapata ajira kwa sababu hana vyeti vya shahada.Source Sulemani Magoma Blog