Social Icons

Sunday 24 June 2012

VYUO VIKUU 60 AFRIKA MASHARIKI KUSHIRIKI MAONYESHO JIJINI ARUSHA





Na.Ashura Mohamed-Arusha
Vyuo vikuu 60
zikiwemo taasisi za elimu ya juu na wadau wa vifaa mbalimbali vya elimu kutoka  nchi za Afrika mashariki  wanatarajia kushiriki katika maonyesho  ya huduma na bidhaa zao yatakayofanyika mwezi
ujao mjini Arusha.

Mratibu wa maonyesho hayo
Peter Oguwi amesema  maonyesho hayo yatakayoanza julai 10 hadi 14 yatafanyika katika viwanja vya nane
nane njiro.

Pia  nyatashirikisha vyuo kutoka nje ya afrika mashariki
ikiwemo India maonyesho ambayo ameyaelezea kuwa ni ya kipekee na mara ya kwanza
kufanyika na yanatarajia kuleta watu zaidi ya 500.

Oguwi amesema
lengo la maonyesho hayo ni kutangaza huduma zinazotolewa na vyuo hivyo zikiwemo
program mbalimbali ilikuwafanya wananchi wanchi hizo kuthamini vyuo vyao badala
ya kukimbilia nchi za nje hivyo maonyesho hayo yana  tarajia kufanya mapinduzi makubwa katika sekta
ya elimu ya juu.

Waziri wa elimu
na ufundi Shukuru kawambwa anatarajiwa kufungua rasmi maonyesho hayo July 11
mwaka huu Jijini Arusha.

No comments: