Social Icons

Wednesday 28 March 2012

MKUTANO WA ELIMU WA UDSM- KUNDUCHI NA UZINDUAIji WA MRADI WA UFUGAJI KUKU DIAMOND JUBLEE

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Philip Mulugo (kushoto) na  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam,  Profesa Rwekaza Mukandala  baada ya kufungua  Mkutano wa Kitaifa kuhusu  Elimu ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwenye hoteli ya Kunduchi  jijini Dar es salaam Machi 28, 2012
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua  Mradi wa  Ufugaji kuku wa Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kwenye ukumbi wa  Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Machi  28,2012. Katikati ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na  Uvuvi, Benedict Ole -Nangoro.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaa baada ya kuzindua  Mradi wa  Ufugaji kuku wa Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Machi  28,2012. Kulia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na  Uvuvi, Benedict Ole -Nangoro. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: