Social Icons

Wednesday 14 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA JENGO LA MIHADHARA LA DUCE M.158 ZACHANGWA KUSAIDIA UJENZI




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuzindua Jiwe la Msingi la Jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, uzinduzi uliambatana na uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari Chang’ombe, ambapo katika zoezi hilo la uchangishaji fedha Makamu alichangia Sh. Milioni 10, na kufanya jumla ya michango kufikia Sh. Milioni 158.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuzindua Jiwe la Msingi la Jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, uzinduzi uliambatana na uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari Chang’ombe, ambapo katika zoezi hilo la uchangishaji fedha Makamu alichangia Sh. Milioni 10, na kufanya jumla ya michango 
kufikia Sh. Milioni 158.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mchango wa sh. 60,000 ulioplewa na watoto wa Shule ya awali ya Duce kutoka kwa mtoto, Edna Mayungi, wakati wa zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya sekondari Chang’ombe lililofanyika wakati wa uzindu wa Jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE leo Septemba 13 jijini Dar es Salaam. Katika zoezi hilo zilipatikana jumla ya Sh. Milioni 158 kwa njia ya ‘Cash’ Ahadi na Mnada. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Terezya Huvisa (kushoto) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, Prof. Salome Misana, baada ya kuzindua rasmi Jengo la Mihadhara la chuo hicho na kuendesha zoezi la uchangishaji fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo Septemba 13

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya chumba cha mihadhara kilichopo katika jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, baada ya uzinduzi uliofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam leo Septemba 13
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia picha yake iliyoandaliwa maalu kwa ajili ya kupigwa mnada katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari ya Chang’ombe, uliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki ch DUCE leo Septemba 13. Katika zoezi hilo zilipatikana Jumla ya Sh. Milioni 158 kwa njia ya Mnada, keshi na ahadi

Watoto wa Shule ya awali ya DUCE, wakiimba ngonjela mbele ya mgeni rasmi, wakati wa uzinduzi huo leo.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: